Kama unaitafuta akaunti ya Instagram ya Fid Q kuanzia jana bila
mafanikio basi fahamu kuwa hackers wameitaifisha, kufuta picha zake zote
na kuigeuza kuwa ya Wema Sepetu.
Akaunti hiyo ina followers zaidi 160,000.
“Account hii imekuwa hacked jana usiku ila mimi nimegundua leo asubuhi,” Fid ameiambia Clouds FM.
“Niligundua baada ya kuingia katika account ikawa inanigomea. Mimi
nilikuwa nimeandika mwanaharakati, sasa naona wameamua kubadili na jina
na kuandika jina la Wema Sepetu,” alisema.
Ok.. Wamehack insta.. Nasubiria wafanye hivyo kwenye hii ya Twitter na Facebook ili niweze ku-enjoy NATURE zaidi… No biggie 🙏
— #KEMOSABE(Interlude) (@FidQ) August 17, 2015
Uzuri ninawajua mliofanya huu upuuzi.. Na kiukweli MNAFELI sana.
— #KEMOSABE(Interlude) (@FidQ) August 17, 2015

Note: Only a member of this blog may post a comment.