Khloe Kardashian.
LOS ANGELES, Marekani
HII ina maana kuwa ndoto za Lamar Odom kurudiana na mkewe Khloe Kardashian, hazipo tena baada ya mrembo huyo kukiri hadharani kuwa hana hisia na staa huyo wa zamani wa NBA.
HII ina maana kuwa ndoto za Lamar Odom kurudiana na mkewe Khloe Kardashian, hazipo tena baada ya mrembo huyo kukiri hadharani kuwa hana hisia na staa huyo wa zamani wa NBA.
Khloe alionekana kutoa msaada mkubwa zaidi kwa Lamar alipopoteza
fahamu akidaiwa kutumia madawa ya kulevya, hali iliyotafsiriwa kuwa
huenda wangerudiana baada ya Lamar kupona.
Mrembo
huyo alisema kwa sasa Lamar atabaki kuwa rafiki na mfanyabiashara
mwenzake huku ikidaiwa kuwa mrembo huyo anataka kuanza tena kufuatilia
talaka yake mahakamani ili aachane naye jumla.
“Sidhani kama nina hisia na Lamar, nilikuwa karibu naye ili
kumhudumia lakini watu wakatafuta sababu za kuongea. Nilitaka Lamar awe
sawa na furaha pia. Kama ulikuwa pamoja na mtu kwa muda mrefu katika
maisha lazima naye atakuwa nawe maishani,” alisema Khloe.
Chanzo kingine kilidai kuwa: “Lamar alitaka kumchumbia tena Khloe
alisema wanataka wairudishe ndoa yao lakini Khloe alikataa akikumbuka
namna alivyomsaliti na sasa anafuatilia talaka ili awe huru kutafuta
mwanaume mwingine wa kumuoa.”
Note: Only a member of this blog may post a comment.