George Michael.
NEW YORK, MarekaniUNAMKUMBUKA George Michael, staa wa ngoma iliyokonga nyoyo za mashabiki kibao enzi zile ya Careless Whisper? Jamaa inasadikika yupo mbioni kurudi kwenye gemu baada ya kupotea kwa muda mrefu kutokana na kutopea kwenye madawa ya kulevya.
Kufuatia kupata huduma za ushauri nasaha, George Michael anarudi. Lakini ngoja tukukumbushe vituko vyake vilivyochangia aadimike kilingeni.
Aprili 1998, George alikamatwa na polisi akifanyiwa mchezo mchafu hadharani kwenye maegesho ya magari na baada ya hapo akautangazia ulimwengu kuwa yeye ni shoga.
Mei 2007, akakiri kosa la kukamatwa akiwa anaendesha gari wakati akijua kuwa amevuta madawa ya kulevya.
Septemba 2008, akaonywa kwa kupatikana na madawa ya kulevya aina ya cocaine na mengine.
Agosti 2010 akakiri kuendesha akiwa amevuta bangi na akafungiwa leseni kwa miezi sita.

Note: Only a member of this blog may post a comment.