Na Richard Bukos
MAHASIMU wawili katika anga la
mastaa, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wiki iliyopita walikwepana na
kushindwa kusalimiana, licha ya wote kuwa waalikwa katika hafla maalum
ya kujipongeza iliyofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Gazeti hili ambalo pia lilikuwepo kwenye
viwanja hivyo vilivyosheheni mastaa wa fani mbalimbali, liliwaona
wawili hao ambao awali walikuwa mar
wemaafiki wakubwa, wakijivinjari kwa tahadhari ili wasikutane, licha ya nyakati tofauti kuzungumza na mastaa wengine.
Wema ambaye katika kampeni za CCM
alikuwa pamoja na Makamu wa Rais, aliyekuwa mgombea mwenza Samia Hassan
Suluhu, wakiwa na kundi lao maarufu la Mama Ongea na Mwanao, muda mwingi
alionekana akiwa na wenzake aliokuwa nao ‘timu moja’ kwenye kampeni.
Aunt Ezekiel ambaye wakati wa kampeni
hizo alikuwa kundi lililopewa jina la Nimestuka, naye alijichanganya na
waalikwa wengine lakini jicho lake likiwa makini kuhakikisha hakutani
hata sehemu moja na muigizaji huyo wa Filamu ya Madam.
Katika sherehe hiyo pia walikuwepo
viongozi mbalimbali wa kitaifa wa serikali iliyopita, akiwemo Waziri
Mkuu Mizengo Pinda na mkewe, mama Salma Kikwete na waziri mkuu wa zamani
wa Kenya, Raila Odinga na mkewe.
Mastaa wengine waliojumuika katika hafla
hiyo iliyochagizwa na muziki kutoka kwa Yamoto Band ni pamoja na
mwanamuziki nguli wa muziki wa dansi, Ally Choki, muigizaji mkongwe, Bi
Mwenda, mlezi wa wasanii Mama Loraa na Emmanuel Mbasha.

Note: Only a member of this blog may post a comment.