MEMBA wa zamani wa Kundi la G Unit, The Game, ameonekana kulimaliza bifu lake na aliyekuwa memba mwenzake ambaye bado yupo kwenye Lebo hiyo, Lloyd Banks baada ya kutupia picha wakiwa pamoja huko Dubai lakini katika hali ya kushangaza, staa 50 Cent ameonekana kutofurahishwa.
The Game na Lloyd Banks walikutana Dubai hivi karibuni na kupiga picha ambayo waliitupia kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram na kuandika “Still”, yaani bado.
Kitendo cha wawili hao kupatana kimeonekana kutomfurahisha 50 Cent ambaye ndiye kiongozi mkuu wa G Unit kwani hana maelewano mazuri na The Game.

Note: Only a member of this blog may post a comment.