Ni stori ambayo ilianza kuchukua headline tangu asubuhi ya Agosti 18, 2015 kuhusu ugonjwa wa kipindupindu mitandao mbalimbali imeripota, sasa saa chache zilizopita nilikwenda kwenye hospitali ya Mwanyamala kuhakikisha.
Taarifa niliyoipata kutoka hospitali ya Mwananyamala kuwa wameshapokea wagonjwa 20 ambao wanahisiwa kuwa na vimelea vya ugonjwa wa Kipindupindu.
Kwa mujibu wa Dkt.Ngonyani’Sasa hivi nimevyoongea tumeshapata wagonjwa 20 wenye vimelea vya ugonjwa wa kipindupindu kati ya hao wagonjwa watatu wamefariki dunia na wagonjwa sita vipimo vyao vimeshatoka na vimethibitishwa kuwa wanavimelea vya ugonjwa vya kipindupindu na waliobaki wanaendelea na matibabu’ – Dkt Ngonyani
‘Ugonjwa wa kipindupindu ni ugonjwa wa hatari sana kwa hiyo mgonjwa anapofika hapa hospitalini tumetenga sehemu maalumu yaani wodi yao maalumu kwaajili ya kupata huduma na kuanza kupata vipimo na pale wanapogundulika kuwa wanavimelea vya ugonjwa wa kipindupindu basi tunawasafirisha kuelekea kwenye kituo maalumu yaani kambi ambacho kipo Mburahati’ – Dkt Ngonyani
‘Sasa ni kuthingatia taratibu za usafi kwanza kunawa mikono yako miwili pale unapotoka chooni, pili hakikisha unapokula matunda yaoshe vizuri, tatu mazingira ya nyumbani yawe safi na salama, nne kuepuka na misongamano ya watu hata sehemu zile ambazo mtu amefariki kuweka matanga haturuhusu kufanya hivyo kwa hiyo kuepuka na hiyo vitu basi tunaweza tukaondoa hili tatizo’ – Dkt Ngonyani
Wodi ya wagonjwa wa kipindupindu.
Note: Only a member of this blog may post a comment.