Mbwana Samatta.
Ibrahim Mussa, Dar es Salaam
TP Mazembe ipo katika harakati
za kumuuza straika Mbwana Samatta kwenda Lille ya Ufaransa, lakini
meneja wa mchezaji huyo, Jamal Kasongo ametoa sharti jipya la nyota huyo
kwa timu atakayoenda.
Kirahisi tu, Kasongo amesema Samatta ni
lazima ajiunge na timu yenye uwezo wa kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya
(Uefa) au Kombe la Europa, ambako anaweza kukutana na Wayne Rooney wa
Manchester United au Santi Cazorla wa Arsenal.
Santi Cazorla
Akizungumza na Championi Jumamosi, Kasongo
alisema mpaka sasa wana ofa kutoka timu za mataifa matano lakini jambo
la msingi kwao ni kuangalia uwezekano wa kucheza katika klabu
inayoshiriki michuano mikubwa Ulaya.
“Bado tupo katika mazungumzo kwa sababu
ofa ambazo mpaka sasa tunazo mezani zinatoka katika nchi za Ujerumani,
Ufaransa, Bulgaria, Hispania na Ubelgiji, ila ukiitoa Bulgaria, nchi
zilizobaki anaweza kucheza.
“Hatuwezi kusema moja kwa moja kama anakwenda Ufaransa kwa sababu tunataka timu ambayo itacheza michuano hiyo ya Uefa na pia iliyo katika hali nzuri kwa masuala ya maslahi.
“Hatuwezi kusema moja kwa moja kama anakwenda Ufaransa kwa sababu tunataka timu ambayo itacheza michuano hiyo ya Uefa na pia iliyo katika hali nzuri kwa masuala ya maslahi.
“Samatta akicheza Uefa au Europa atakuwa
amefika mbali sana na atajitangaza yeye mwenyewe na Tanzania kwa jumla
hivyo ni lazima tuliangalie hilo kwanza,” alisema Kasongo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.