Marehemu Geofrey enzi za uhai wake.
Na Makongoro Oging’
MADAI MAZITO! Jeshi la Polisi Mkoa wa
Kinondoni, Dar limesema linamshikilia mwanadada Rhoda Daudi kwa tuhuma
ya kumuua kwa kumchoma kisu, Geofrey Valeli Kapulula (37) aliyetarajia
kufunga naye ndoa hivi karibuni, Uwazi lina mkasa wote.
Tukio hilo la kutisha na ambalo limeacha maswali, lilijiri
maeneo ya Ubungo National Housing (NHC) jijini Dar es Salaam, Novemba
23, mwaka huu.
Bi harusi anayetuhumiwa kwa kosa la kumchoma kisu Geofrey.
UWAZI ENEO LA TUKIO
Mwandishi wa habari hii, alifika katika eneo la tukio na kuzungumza na majirani ambao walisema kwamba siku ya tukio walisikia sauti ya marehemu akiomba msaada lakini hata hivyo, hawakujali kutokana na kuzoea wawili hao kugombana mara kwa mara na kisha kupatana.

Mmoja wa majirani hao ambaye hakupenda jina lake kuandikwa gazetini,
alisema siku ya tukio, wapendana hao walikuwa wakinywa kwenye baa moja
na marafiki zao huku wakibadilishana mawazo lakini kukatokea ugomvi kati
ya marehemu na mtuhumiwa ambapo ilipofika saa tatu usiku mwanamke
akaondoka kurudi nyumbani huku mwanaume akibaki na kurejea nyumbani
baadaye.
CHANZO CHA UGOMVI
“Walipofika nyumbani ugomvi uliendelea. Sauti ya Rhoda ilisikika akiitaka simu ya Geofrey kwa madai ilikuwa na ujumbe wa mapenzi kwenye Mtandao wa WhatsApp kutoka kwa mwanamke mwingine.”
“Walipofika nyumbani ugomvi uliendelea. Sauti ya Rhoda ilisikika akiitaka simu ya Geofrey kwa madai ilikuwa na ujumbe wa mapenzi kwenye Mtandao wa WhatsApp kutoka kwa mwanamke mwingine.”
MADAI MENGINE
Madai mengine yanasema kuwa, wakati Geofrey akiwa anatapatapa nje kwa jeraha la kisu, Rhoda alimpigia simu ndugu mmoja wa marehemu huyo (jina tunalo) na kumjulisha kuwa amemchoma kisu Geofrey na kwamba ana hali mbaya kiasi cha kufa.

Jeneza lililobeba mwili wa marehemu likiandaliwa kwa ajili ya kuagwa.
Inadaiwa kuwa, baada ya kifo hicho, ndugu huyo alihojiwa na polisi na
kuanika ukweli wa simu aliyopigiwa na Rhoda. Hata hivyo, mamlaka za
kisheria hazijathibitisha juu ya kuwepo kwa mawasiliano kati ya ndugu
huyo na Rhoda.
MTOTO WA MWENYE NYUMBA NA UWAZI
Naye Justice James ambaye ni mtoto wa mwenye nyumba aliyokuwa akiishi marehemu, alipohojiwa na gazeti hili kuhusu sakata hilo, alisema haya:
Naye Justice James ambaye ni mtoto wa mwenye nyumba aliyokuwa akiishi marehemu, alipohojiwa na gazeti hili kuhusu sakata hilo, alisema haya:
“Siku hiyo, nakumbuka kwenye saa tisa usiku, nilisikia sauti ikiita
kwa kutaka msaada. Nilipotoka nilimkuta Geofrey amelala chali nje karibu
na ngazi za kuingilia ndani. Alikuwa akikoroma tu!
“Nilimuuliza nini kimempata, akashindwa kuniambia, aliendelea kukoroma huku amelowa damu. Niliamua kuwaamsha majirani wengine.”
Mmoja wa waombolezaji akilia kwa simanzi kubwa.
JERAHA LA KISU LAONEKANA
“Nikiwa na majirani, tulimkagua Geofrey ambapo tulimkuta na jeraha begani karibu na shingo upande wa kushoto. Tulimchukua na kumweka kwenye gari langu ili kumkimbiza Hospitali ya Palestina (Sinza). Pale tulikuta geti limefungwa, tukampeleka Hospitali ya Mwananyamala ambako daktari alisema alishafariki dunia.”
HISTORIA YA MTUHUMIWA
“Mtuhumiwa (Rhoda) alipanga hapa kwetu Aprili, mwaka huu na alitutambulisha kuwa, Geofrey ni mchumba’ake ambaye wangefunga ndoa hivi karibuni.”

MAMA MWENYE NYUMBA
Mama mzazi wa Justice, Juliana Benedict ambaye alikuwa akilia mara kwa mara kutokana na mauaji hayo ya kikatili, alisema wapangaji wake hao aliwapenda sana na aliwachukulia kama watoto wake.
Mama mzazi wa Justice, Juliana Benedict ambaye alikuwa akilia mara kwa mara kutokana na mauaji hayo ya kikatili, alisema wapangaji wake hao aliwapenda sana na aliwachukulia kama watoto wake.
KAKA WA MAREHEMU
Naye Denis Kapulula alisema ni kaka wa marehemu, yeye kwa upande wake alisema alipata taarifa ya kifo cha mdogo wake siku hiyo usiku na kwenda katika eneo la tukio ambapo alikuta polisi na baadhi ya majirani.

….Mwili wa marehemu ukiagwa.
“Tulipata taarifa kuwa, mzozo mkubwa ulikuwa ujumbe katika simu ya
marehemu, mtuhumiwa namfahamu, hata nyumba waliyokuwa wakiishi, mdogo
wangu ndiyo alikuwa akilipa kodi. Mdogo wangu alishawahi kuoa huko
Salasala alikojenga, akazaa mtoto mmoja, lakini walitofautiana na huyo
mke, ndiyo akawa na mtuhumiwa,” alisema Denis.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Camillius Wambura amekiri jeshi lake kumshikilia Rhoda kwa tuhuma za kumuua Geofrey.
“Ni kweli tunamshikilia Rhoda kwa tuhuma za kumuua kwa kisu, Geofrey.
Upelelezi bado unaendelea,” alisema Kamanda Wambura.Marehemu Geofrey
alizikwa Novemba 26, mwaka huu kwenye Makaburi ya Mbezi Kibanda cha Mkaa
jiijini Dar.

Note: Only a member of this blog may post a comment.