Wasomali wakiwa chini ya ulinzi.
Makongoro Oging’ na Issa Mnally
WAMENASWA! Jeshi la Polisi Kituo cha Buguruni kwa kushirikiana na Serikali ya Mtaa wa Machimbo, Kata ya Segerea, Ilala jijini Dar es Salaam wamewanasa watu 105 raia wa Somalia wakidaiwa kuwa safarini kwenda nchini Afrika Kusini, Uwazi linakupa kwa undani.
WAMENASWA! Jeshi la Polisi Kituo cha Buguruni kwa kushirikiana na Serikali ya Mtaa wa Machimbo, Kata ya Segerea, Ilala jijini Dar es Salaam wamewanasa watu 105 raia wa Somalia wakidaiwa kuwa safarini kwenda nchini Afrika Kusini, Uwazi linakupa kwa undani.
Tukio hilo la kushangaza lilitokea saa 11 alfajiri ya Alhamisi
iliyopita kwenye nyumba ya kigogo mmoja aliyekuwa mfanyabiashara mkubwa
Dar (jina lipo) ambaye ni marehemu. Nyumba hiyo iliyopo Tabata Segerea
kwa sasa inasimamiwa na mtoto wa marehemu aitwaye Mariam.
Polisi wakiwa katika eneo la tukio.
Waadishi wa habari hii walifika eneo la tukio muda mfupi baada ya
kukamatwa kwa watu hao ambapo zoezi hilo lilikuwa likiongozwa na Mkuu wa
Upelelezi Wilaya ya Kipolisi Buguruni, Ibrahim Nkindwa na Mkuu wa Kituo
cha Polisi Tabata Shule, Bakar Goti baada ya kutonywa kuwepo kwa watu
hao katika nyumba hiyo iliyopangishwa kwa Zabibu Umwiza raia wa Burundi
ambaye ndiye anadaiwa kuwahifadhi watu hao.
ainabu alikimbia baada ya polisi kufika na silaha za moto.
Kwa mujibu wa shuhuda mmoja, kugundulika kwa Wasomali hao kulifuatia kuwasili kwa lori moja kwenye nyumba hiyo usiku wa saa tisa.
Kwa mujibu wa shuhuda mmoja, kugundulika kwa Wasomali hao kulifuatia kuwasili kwa lori moja kwenye nyumba hiyo usiku wa saa tisa.
….Wakiwa kwenye basi la polisi.
“Baada ya lori kufika usiku huo, geti likafunguliwa. Halafu kukaanza
kusikika vishindo vya tii…tii…tii! Kumbe jamaa (Wasomali) walikuwa
wakiruka chini mmojammoja kutoka kwenye lile lori na kuingia ndani.
“Ndipo jirani mmoja aliamua kutoa taarifa polisi ambao walifika na
kuwakuta jamaa wamerundikana ndani kwenye vyumba tofauti. Mia moja na
tano ni wengi sana,” alisema shuhuda huyo.
Akaendelea: “Tuna shaka hawa watu, wengine ni Al-Shabaab. Hii hali
inatia wasiwasi sana. Je, kama wamepita na silaha nzito na wamezificha
sehemu? Itakuaje? Hawa Uhamiaji wa mipakani waangaliwe sana.”
Nyumba walimokutwa wasomali hao.
Mariam anayesimamia nyumba hiyo, anaishi Magomeni, Dar alipofika
alishangaa kwa tukio hilo la mpangaji wake kuwahifadhi watu hao, hasa
kutokana na idadi yao kuwa kubwa.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo, Mariam Mchicha naye alikuwa mstari wa mbele katika zoezi hilo la kamatakamata.
Aliitupia lawama Idara ya Uhamiaji na kusema ina matatizo makubwa
kutokana na kuwapitisha au kuwepo kwa uzembe wa kuwabaini watu hatari
ambao baadaye wanaweza kuleta matatizo makubwa nchini.
….Moja ya chumba walichokuwa wakilala.
“Nalipongeza Jeshi la Polisi Buguruni kwa kazi nzuri ya kiupelelezi
na kuweza kuwagundua watu hawa, ninapenda kuwaasa wananchi kutoa taarifa
katika vyombo vya serikali watu wanaowatilia shaka ili wakamatwe,”
alisema kiongozi huyo.
Watu hao walichukuliwa katika basi kubwa la polisi huku
likisindikizwa na king’ora hadi Kituo cha Polisi Buguruni kwa mahojiano
zaidi.

Note: Only a member of this blog may post a comment.