Wednesday, November 18, 2015

Anonymous

UPDATES: Zoezi la Kuapishwa Wabunge Wateule Laendelea

Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeendelea na zoezi la kuwaapisha wabunge wateule mbele ya Spika Job Ndugai.
Kiapo cha wabunge hao ni ishara ya kupokea na kuanza majukumu yao ya kuwawakilisha wananchi.

Hiki ni kikao cha pili cha Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Zoezi la kuapishwa wabunge wateule limeanza majira ya saa tatu asubuhi baada ya kuahirishwa jana.

Baadhi ya wabunge waliopata nafasi ya kuapishwa asubuhi ya leo wamekula kiapo cha utii na uaminifu kuonyesha utayari wa kuwatumikia wananchi.

Bunge limeahirishwa saa tano kamili asubuhi hadi saa 11 jioni ambapo linaendelea na zoezi la kuwaapisha wabunge wateule waliobaki.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.