Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu na
Mbunge wa jimbo la Mikumi Mhe. Joseph Haule a.k.a Professor Jay, ni
wasanii wa muziki ambao wamefanikiwa kuingia kwenye Bunge la 11 baada ya
kushinda kwenye uchaguzi wa mwaka huu.
Kupitia 255 ya XXL Sugu ambaye alikuwa Mbunge kwenye bunge
lililopita, amempa ushauri Professor ambaye ndio ameingia mjengoni kwa
mara ya kwanza kuhusu malalamiko kutoka kwa wasanii.
“Unajua wasanii wamekuwa wakilalamika kuhusu uwepo wangu mjengoni,
ngoja niseme kitu kwa Proffesor Jay, naomba atambue yeye ni Mbunge wa
Mikumi na hakuna jimbo la Wasanii, kama mimi nilivyo Mbunge wa Mbeya
Mjini. Tufanye kazi kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi wetu
waliotuchagua. Kwa sababu Wasanii wamekuwa na tabia ya kuongea kuwa
tunashindwa kuwasaidia sisi sio wabunge wa Wasanii naomba ieleweke”.
alisema Sugu.
Sugu aliendelea;
“Kuna Wasanii wengine walikuwa hawakupi hata support kipindi cha
Kampeni ila ukishinda na ukaingia bungeni, ndio wa kwanza kukutupia
lawana.”
Note: Only a member of this blog may post a comment.