Bado headlines za usajili wa dirisha
dogo bado zinachukua nafasi kwa wachezaji kadhaa kuhusishwa kujiunga na
vilabu fulani na wengine kutemwa na vilabu vyao kutokana na
kutoridhishwa na viwango vya wachezaji hao. November 18 klabu ya Simba imetangaza kuwatema wachezaji wawili wa kimataifa

Pape N’daw
Pape N’daw
Simba ambayo ilikuwa inatajwa kwa karibu kumtema Pape N’daw aliyetokea Senegal na mchezaji mmoja mwingine wa kigeni, imethibitisha leo November 18 kuwatema wachezaji wawili Simon Sserunkuma kutoka Uganda na Pape N’daw kutokea Senegal aliyeitumikia klabu hiyo kwa nusu msimu na kocha wa Simba Dylan Kerr kupendekezwa aachwe kutokana na kutoridhishwa na uwezo wake.
Kupitia kwa Afisa Habari wake Haji Manara wametangaza kuwatema wachezaji hao na kumrejesha Paul Kiongera aliyekuwa anaichezea KCB ya Kenya kwa mkopo. Hata hivyo mmoja kati ya wanachama wa Simba amemleta mchezaji kutoka Cameroon Doumbie Ernest aliyekuwa anaichezea Leopard FC ya ligi daraja la pili Cameroon usiku wa November 17 kwa ajili ya majaribio Simba.
Doumbie Ernest kutoka Cameroon aliyekuja kufanya majaribio Simba wakati wa exclusive interview na millardayo
“Simba
imeachana na Pape N’dawa na Simon Sserunkuma kutokana na mapendekezo ya
benchi la ufundi hususani mwalimu Kerr ila katika kuacha huko Simba
inamrejesha mchezaji wake Paul Kiongera aliyekuwa kwa mkopo KCB ya Kenya
na inaweza kusajili mchezaji mwingine” >>> Manara
Sauti ya Haji Manara na Doumbie Ernest zipo hapa mtu wangu.
Note: Only a member of this blog may post a comment.