Friday, November 20, 2015

Anonymous

MSIBA: Mtangazaji Maarufu Nchini, Prince Baina Kamkuru Afariki Dunia Ghafla Jijini Dar

Prince Baina Kamkuru enzi za uhai wake.
Mtangazaji wa zamani wa Radio Free Afria (RFA), Clouds FM na Star TV, Prince Baina Kamkuru amefariki dunia ghafla jana usiku akiwa jijini Dar es Salaam. 

Taarifa za awali kuhusu kifo cha marehemu Kamkuru zinaeleza kuwa alianguka ghafla wakati akifanya mazoezi ya viungo na alipokuwa akiwahishwa hospitali kwa matibabu alifariki dunia.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda mkoani Kagera kwa mazishi siku ya Jumapili na kwa sasa msiba upo Kigamboni jijini Dar.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.