
Tanzania bado iko kwenye majonzi baada ya msiba wa aliyekuwa mbunge wa Ludewa,Deo Haule Filikunjombe pamoja na Rubani Captain William Silaa na watu wengine wawili Egid Nkwera pamoja na Cassablanca Haule waliofariki kwenye ajali ya Helikopta kwenye mbuga ya Selous.
Najua
kuna watu walikuwa na maswali juu ya atakayewaongoza wakazi wa Ludewa,
sasa leo Novemba 5, 2015 mke wa marehemu Deo Filikunjombe ‘ Saraha’
ameyaandika maneno haya hapa chini kupitia akaunti yake ya instagram kuhusiana
aliyeteuliwa kugombea jimbo la Ludewa.
‘Nawaombeni
wana ludewa wote kwa heshima nawaomba niwaambie ukweli kuwa huyu ndie
anayeweza kuvaa viatu vya mume wangu mpendwa kwani mara nyingi amewahi
kumchangia kaka yake ada za watoto tuliokuwa tunawasomesha huko ludewa
naombeni msidanyike na maneno ya hao wagombea wengine mbona leo ndo
wamekuja ludewa walikuwa wapi kujakuleta maendeleo mpaka iwe baada ya
deo kufariki kati ya wagombea wote hakuna rafiki wa mume wangu’ – Saraha

Note: Only a member of this blog may post a comment.