Ukizungumzia viwanja vikubwa vya soka duniani Wembley, The Nou Camp, The Maracana, The San Siro, Bernabeu. Allianz Arena havikosekani.
Lakini watalaam wamekuja na utundu mwingine na kuufanya uwanja huu wa
mpira uliopo Norway kuwa wenye mvuto zaidi duniani kwa muonekano wake.
Huu ni uwanja ambao hauna majukwaa ya mashabiki na unatumika kwa wachezaji wanaocheza soka la ridhaa.
Unaweza ukaona mandhari yake na kukufanya kujiuliza maswali mengi
ikiwemo ni vipi unamudu kuchukua watazamaji wachache kwa wakati mmoja
kutokana na kuwa katikati ya bahari.
Tazama hapa jinsi wachezaji na watazamaji wachache wanavyokuwa huru kutumia uwanja huu..

Note: Only a member of this blog may post a comment.