PROF MUHONGO ATUNUKIWA TUZO:
Taasisi ya Tanzania Awards International Ltd, imemtunuku tuzo ya mwanasiasa mwenye mafanikio katika siasa za Tanzania, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo.
Waandaaji wa tuzo hizo zilizotolewa jana na Rais Jakaya Kikwete kwenye ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere International Conversion Centre (JNICC) wanasema Prof. Muhongo ameshinda tuzo hiyo baada ya kukidhi vigezo vilivyowekwa sambamba na kura nyingi alizopata kutoka kwa watanzania waliopiga kura kupitia zoezi lililoendeshwa na kampuni ya Push Mobile.


Note: Only a member of this blog may post a comment.