Sanchez (kulia) akishangilia moja ya mabao yake.
Kipa wa Arsenal, Petr Cech akiokoa mpira uliopigwa na Bastian Schweinsteiger.
Per Mertesacker (juu) akikwaana na Wayne Rooney wa Manchester United.
MABAO mawili yaliyofungwa na Alexis Sanchez
na moja la Mesut Ozil yametosha kuipa ushindi wa mabao 3-0 timu ya
Arsenal dhidi ya Manchester United katika mechi ya Ligi Kuu ya England
iliyopigwa kwenye Uwanja wa Emirates jioni hii.
Mabao yote ya Arsenal yamefungwa katika
kipindi cha kwanza na kwa ushindi wa leo timu hiyo imefikisha pointi 16
ikiwa nafasi ya pili nyuma ya Manchester City wenye pointi 18 baada ya
kucheza michezo 8.
Vikosi:
Arsenal: Cech, Bellerin, Mertesacker, Gabriel, Monreal; Coquelin, Cazorla; Ramsey, Ozil, Sanchez; Walcott
Manchester United: De Gea, Young, Smalling, Blind, Darmian, Carrick, Schweinsteiger, Mata, Rooney, Memphis, Martial

Note: Only a member of this blog may post a comment.