MARIO Balotelli ana vituko sana Ulaya, lakini Haruna Moshi ‘Boban’, haishi vituko Tanzania.
Boban sasa ni mshambuliaji mpya wa Mbeya
City, timu aliyojiunga nayo siku chache kabla ya kwenda Dubai, Falme za
Kiarabu (UAE) kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka la
kulipwa, lakini akaishia kuswekwa lupango.
Boban aliondoka nchini wiki kadhaa zilizopita kwenda Dubai, baada tu ya kuwasili, mambo yakawa mabaya baada ya maofisa wa uhamiaji kumuweka ndani kutokana na matatizo yaliyojitokeza katika pasi yake ya kusafiria.
Habari za uhakika za uchunguzi kutoka Dubai zimeeleza, pasi ya kusafiria ya Boban ilionekana ilishafutwa.
“Ilishangaza baada ya ‘system’ kuonyesha paspoti yake ilishafutwa. Kukawa kuna utata kweli, ikabidi awekwe ndani,” alisema Mtanzania ambaye anaishi Dubai ambaye alishirikiana na baadhi ya watu kumtoa Boban lupango.
“Tungeweza kumtoa mapema, lakini akiwa ndani iligundulika kuna tatizo jingine. Kwamba namba za paspoti hiyo zilikuwa zikifanana na ile inayotumiwa na Juma Kaseja. Ikawa shida zaidi na hata kumtoa mara moja ikawa shida.”
Taarifa nyingine kutoka Dar es Salaam, zilifafanua kuhusiana na makosa hayo hivi:
2-Kosa la pili halikuwa lake, ila watu wa uhamiaji walichanganya namba kwa kuwa pasi mbili za Boban na ile ya Kaseja zilitolewa pamoja na kusababisha hali hiyo ya sintofahamu.
Mpashaji kutoka Dubai anaeleza, baadaye Boban alitolewa na kuruhusiwa na kuendelea na majaribio, hata hivyo alishindwa kutokana na kuonekana hakuchangamka.
Hali hiyo inaelezwa kuchangiwa na hali iliyotokea. Badala ya Boban, timu hiyo ilisajili kiungo kutoka Brazil.

Note: Only a member of this blog may post a comment.