Wednesday, December 21, 2016

Unknown

Video+Pichaz: Watu 29 Wapoteza Maisha Kufuatia Mlipuko wa Fataki Mexico

Milipuko imelikumba soko la fataki maarufu lililopo kaskazini mwa Mexico City Jumanne na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 29 na kusababisha moshi mkubwa.
Watu 72 wamejeruhiwa, kwa mujibu wa gavana wa jimbo la Mexico, Eruviel Avila.
Chanzo cha mlipuko huo hakijajulikana bado. Mji wa Tultepec unafahamika kwa viwanda vyake vya mafataki na soko la San Pablito ni maarufu kwa uuzaji wa fataki.
Soko hilo lilikuwa na watu wengi kutokana na watu wengi kununua fataki kwaajili ya sikukuu za Christmas na Mwaka Mpya.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.