WAKATI fukuto la chini chini la kisiasa dhidi ya Tanzania na Rwanda likiwa limepoa kama si kuisha kabisa, mapya yameibuka.
Mwanaharakati mashuhuri wa kisiasa
nchini,ambaye alijizolea umaarufu katika bunge la katiba na kipindi cha
uchaguzi mkuu, Humphrey Polepole amedai kuwa pamoja na nchi ya Rwanda
kuwa na mengi ya kujifunza lakini haoni kama kuna baadhi ya mambo kwa
watanzania kujifunza kutoka kwao.
Polepole ambaye anasifika kwa ‘kukomalia
ukweli’ amesema kuwa kitu pekee kinachomvutia nchini Rwanda ni kuona
jinsi wanyarwanda wanavyopiga kazi tu.
Siungi mkono mambo kadhaa kuhusu Rwanda ila kuna mambo tunaweza jifunza kutokwa kwao. Jamaa wanajituma, wengi wetu wavivu. #MshauriMwelekezi
Note: Only a member of this blog may post a comment.