Aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji wa Uingereza BBC, Kassim Kayira.
Kassim Kayira na Idd Seif wakiwa katika studio ya BBC.
Idd Seif na Kassim Kayira wakiagana.
Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji wa Uingereza BBC wakiwaaga watangazi hao.
Watangazaji bora kabisa wa Shirika la Utangazaji wa Uingereza BBC,
katika kipindi cha Dira ya dunia, Kassim Kayira na Idd Seif wameacha
kazi katika kituo hicho kikubwa duniani.
Kwa mujibu wa watangazaji hao wawili waliokuwa pamoja studio katika
kipindi cha Dira ya Dunia kwa mara ya mwisho jana, walisema wameamua
kuacha kazi na kurudi nyumbani Afrika ili kuendeleza miradi yao.
Idd Seif, ambaye alijiunga na BBC mwaka 1997 akitokea Kampala,
Uganda, alisema ameamua kurejea Uganda ili aweze kusimamia miradi yake,
baada ya kazi ya utangazaji kwa miaka 40. Alielezea huzuni yake kwa
kuwaacha watu waliompokea vizuri na kufanya nao kazi kwa miaka 20.
Kwa upande wake, Salim Kayira, alisema alijiunga na shirika hilo
akitokea kituo cha televisheni cha Rwanda miaka kumi iliyopita akiwa
Mhariri. Alisema naye atarejea Afrika ambako atajishughulisha na kilimo
pamoja na ufugaji na sehemu aliyoamua kuishi ni Uganda.
Watangazaji hao wameondoka miezi michache baada ya mtangazaji
mwingine mahiri wa Kiswahili, Charles Hilary wa Tanzania kuacha kazi na
kujiunga na kituo cha televisheni cha Azam. Taarifa ambazo
hazijathibitishwa, zinasema wawili hao nao huenda wakajiunga na Azam tv.

Note: Only a member of this blog may post a comment.