Brighton Masalu
MWIMBAJI nyota wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando
amepatwa na gonjwa la ajabu ambalo licha ya kumtesa kila siku, lakini
vipimo katika hospitali anazokwenda mjini Dodoma, havioneshi kitu gani
hasa anaumwa, Risasi Mchanganyiko lina habari kamili.
“Naumwa
sana, sasa ukichanganya na maneno ya watu, basi najikuta naumia mara
mbili, nimezunguka hospitali mbalimbali, lakini hawaoni ugonjwa wa moja
kwa moja, zaidi ya kupewa dawa za kutuliza maumivu tu, natokwa na
vipele, vinawasha kweli, wakati mwingine ni kama ninachomwa sindano,
vikikauka vinaacha alama nyeusi na kuharibu muonekano wa mwili wangu,
yaani naumwa kweli, nahitaji tu maombi yenu, nitakufa jamani,” alisema
mwimbaji huyo.
Licha
ya maumivu hayo ya mwili, pia mwimbaji huyo alisema kitu kingine
kinachomuumiza ni maneno ya watu juu yake ambayo wakati mwingine hayana
ukweli wowote kama kumsema juu ya magonjwa na vitendo ambavyo hana.
Kutokana na hali hiyo, Rose alisema amekuwa akitumia muda mwingi
kukaa ndani ili kujiepusha na maumivu ya alichokiita ‘masimango ya
walimwengu’ na anapotoka ni kwa ajili ya kwenda kanisani pekee.
Note: Only a member of this blog may post a comment.