Watu wengi wanatamani wawe wajasiriamali au wawe wafanyabiashara na
wakati mwingine wameweza kukurupuka na kuingia kwenye biashara kichwa
kichwa na wanakimbia.
Kuna vitu ambavyo viko wazi na vinahitajika kujulikana kwa kila anayetamani kufanya biashara, inawezekana hakuna mtu anayekuambia kuhusu hivyo vitu ila leo unatakiwa mtu kuvijua kwa undani wake na umuhimu wake.
Nimejaribu kufuatilia vibanda au ofisi nyingi za biashara ndogo au za kati zinapoanzishwa utagundua kuwa mtu ana mtaji wa kiasi fulani ambao utamsaidia kulipa pango, kukarabati eneo hilo na kununua vifaa mbalimbali vya kuanzia na biashara inaanza kwa spidi ya ajabu. Baada ya muda si mrefu unashtukia ile kasi inapungua kwa spidi ya aina yake, kama huduma zilikuwa bora unaona viwango vinaanza kushuka na wafanyakazi kukimbia au kupunguzwa n.k.
Kama unafungua biashara kwa mara ya kwanza unatakiwa kujua kuwa mtaji wa vitu na kulipa pango la biashara si kitu pekee unachohitaji bali unahitaji fedha ya kujiendesha kwa muda wa miezi kadhaa (mfano sita hadi mwaka mzima) ili biashara iendelee kuonekana katika kiwango ulichoanza nacho.
Hapa namaanisha kama una wafanyakazi wawili, hakikisha una hela ya kuwalipa kwa mwaka mzima na gharama ndogo ndogo za ofisi kwa mwaka mzima au miezi sita kusionekane kutetereka katika biashara yako hata kama hakuna wateja. Usitegemee ukifungua biashara utapata wateja papo hapo na hela itarudi, hapana inakuchukua muda kuhakikisha mambo yaende sawa. Ndio maana biashara ili ikue na kustahimili inahitaji miaka mitano ikipita hapo hiyo biashara haiweze kufa ikifa ni kwa uzembe wa wanayoiongoza.
katika kipindi hicho cha kuanza biashara mapato yako au maisha yako yasitegemee biashara hiyo kwani hauna uhakika wa mwenendo mzima wa pesa utakwendaje. Unahitaji sehemu nyingine tofauti na biashara hiyo ambayo itakuingizia kipato cha kuhakikisha unaisimamia biashara hiyo mpaka inainuka kabisa.
Kitu kingine usitumie fedha yote katika kununua mzigo, unahitaji kiasi fulani cha fedha ambacho hakiguswi kinasubiri dharura katika biashara hiyo. Fedha hiyo inasaidia kuishikiria biashara endapo kuna kitu kitayumba au kuharibika. Kumbuka viwango ulivyoanza navyo ndio unatakiwa kuendelea navyo, unahitaji kufikiria kabla vitu havijatokea katika biashara, mfano wizi, moto, kudhulumiwa n.k!

Note: Only a member of this blog may post a comment.