Pamoja na kukanusha kwa nguvu zote, staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul
‘Diamond Platnumz’, anadaiwa kupandiwa kichwani na mwandani wake,
Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ huku ndugu wakidaiwa kuhofia masuala
ya kulishwa limbwata.
Staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Habari kutoka kwa mtu wa ndani wa familia
ya Diamond zilidai kuwa, ishu hiyo imekuwa ‘hoti’ kiasi cha kuwatia hofu
ndugu hao kwa sababu Zari akisema jambo lazima Diamond
alitekeleze.“Hata ishu ya kuondoka kwenda kwao Afrika Kusini ‘Sauz’
akiwa na mtoto wao mchanga (Tiffah) ilikuwa ghafla sana na wala Diamond
hakuweza kubisha.
“Kuna mambo mengine kibao ambayo Diamond alikuwa anamfanyia Zari
ikiwemo kumpikia wakati yeye akichati kwenye simu na mambo mengine
yanayofanana na hayo,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
...Akipika.
“Asikwambie mtu, Diamond hafurukuti mbele ya Zari maana mwanamama
huyo kampanda kichwani. Kuna wengine wanahusisha ‘situwesheni’ hiyo na
umri maana Diamond katimiza umri wa miaka 26 juzikati wakati Zari
kagonga 35.”Akizungumzia hali hiyo, Diamond alifunguka kwa kifupi: “Nilishasema hayo ni mapenzi tu lakini Kibongobongo si unajua watu hawana dogo?”
Note: Only a member of this blog may post a comment.