Monday, August 24, 2015

Anonymous

Sikupenda kuona Nuh Mziwanda akimtongoza bosi wangu WEMA – Mirror

Msanii wa Endless Fame Films, Mirror amesema alimrekodi Nuh Mziwanda wakati akimtongoza bosi wake Wema Sepetu sababu hakupendezwa na kitendo hicho alichokiona kama ni utovu wa nidhamu.
11311556_123122804697601_1275150369_n
Akizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live cha EATV, Mirror alisema hawezi kufurahi kumuona ‘dogo’ tu akimtongoza bosi wake.
“Mimi sina matatizo na Nuh cha kwanza na sikurekodi kwa nia ya watu wasikilize,” alisema. “Kwa sababu hata tukiongea ukweli Nuh na madam ni vitu viwili tofauti, [Wema] ni boss, mkubwa hata kwangu. Mimi nilikuwa naangalia movies na sikurekodi kwa nia hata kama akija kusikia girlfriend wake ajue Nuh ndio alikuwa anamsumbua madam,” aliongeza.
11311537_489713927859370_1121246852_n Mirror akiwa DJ Ommy Crazy na Sam Misago wa EATV
“Sijawahi kusikia mtu mwingine akimtongoza madam, siwezi kufurahi Nuh akimtongoza bosi wangu kwa sababu yeye ni dogo kama mimi, halafu yeye ana mwanamke wake pia.”

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.