Saturday, September 12, 2015

Anonymous

Ukiamua, ‘Viatu’ vya Bilionea BAKHRESA Vinakutosha Kabisa!

AzamBakeriesx700Maisha ya sasa yana changamoto nyingi sana, wanaoweza kuishi kwa furaha ni wale ambao kila siku wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii wakiwa na dhamira ya dhati kabisa ya kuyaboresha maisha yao.
AzamSoftdrinkx700-2Achilia mbali hao ambao wanapambana kuyaboresha maisha yao, wapo ambao wamekuwa wakiota kuwa na mafanikio makubwa sana. Wamekuwa wakiumiza vichwa juu ya nini wafanye ili mwisho wa siku wawe miongoni mwa wale waliofanikiwa.
Hawa ni wale wanaojua maana halisi ya maisha. Wanaojua kuwa mafanikio ni kwa kila mtu na kwamba anayeishi ili mradi siku zinakwenda, hawezi kuwa na faida yoyote kwenye jamii anayoishi.

Wenye mawazo hayo ndiyo wale ambao siku hadi siku huona mabadiliko katika maisha yao. Wanaaga umasikini kwa kasi ya aina yake. Mimi na wewe tunatakiwa kuwa hivyo. Kuamini kwamba maisha ya kuwa na uhakika wa kula, kulala na kuvaa vizuri tu siyo tuliyopangiwa.

Maisha sahihi tuliyopangiwa ni kuwa na uhakika wa kujipatia mahitaji hayo muhimu lakini pia kuwa na ziada ambayo itatufanya tuwasaidie wale ambao hawana uwezo.

Lakini sasa, wakati wewe na mimi tukiwa kwenye jitihada za kusaka mafanikio, wapo watu ambao wanashangaza sana. Nawazungumzia wale ambao wana tabia ya kuwakatisha tamaa wenzao wenye uchu wa mafanikio.

Watu hawa wapo huko mtaani. Unakuta wewe unapambana kutimiza ndoto zako, anatokea mtu ambaye ameshajikatia zake tamaa, anakuvunja moyo ili tu uone kwamba huwezi kufikia pale unapopataka.

Usishangae mtu akakuambia, ‘….wa kufanikiwa utakuwa wewe bwana’. Sasa unabaki kujiuliza, kwa nini wa kufanikiwa usiwe wewe wakati mafanikio yamewekwa kwa kila mtu? Baadaye ndipo wewe mwenye uelewa utagundua kuwa, maneno uliyoambiwa yana lengo la kukukatisha tamaa.

Kwa bahati mbaya sana, maneno hayo yanaweza kumkuta mtu ambaye uelewa wake ni mdogo, akachukulia kwamba ni kweli hawezi kufanikiwa, matokeo yake anaanza kurudi rivasi, zile ndoto za kuwa na mafanikio makubwa zinayeyuka.

Ndiyo maana inashauriwa kuwa makini sana na watu wanaokuzunguka. Jitahidi kuwa karibu na wale ambao wanaenda sawa na dhamira yako, wale wanaokushauri namna ya kufikia mafanikio makubwa, jinsi ya kukabiliana na changamoto pamoja na kukutia moyo pale ambapo unakwama.

Epukana na watu ambao wanaonekana dhahiri hawataki kukuona ukifanikiwa. Hawa ndiyo wale ambao usishangae hata wakakuendea kwa waganga eti ili tu usifanikiwe.
Pointi ya msingi leo ni kwamba, mimi na wewe tuna kila sifa ya ‘kuvaa viatu’ vya akina Bakhresa na Bill Gates lakini hatujui hilo. Matokeo yake tunawapa nafasi watu walioshindwa na maisha watukatishe tamaa. Tukiwa hivyo tutakuwa tunakosea sana.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.