Monday, September 7, 2015

Anonymous

Sumu ya DK SLAA Yavuruga Mafuriko ya UKAWA

6...SlaaakizungumzajambombeleyawanahabarijuuyahatmayakeyakuachananaChamaChaDemokrasianaMaendeleo..JPGAliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa.
Mwandishi wetu
‘SUMU’ inayomwagwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa dhidi ya mgombea urais wa chama hicho, Edward Lowassa juu ya madai ya ufisadi, yanavuruga kwa kiasi kikubwa ‘mafuriko’ ambayo yamekuwa yakionekana katika mikutano ya kampeni.
Lowassa (6)Mgombea urais wa Ukawa, Edward Lowassa.
Kabla ya kuibuka kwa Slaa, Lowassa alikuwa kivutio kikubwa kwa wanachama na wafuasi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wanachi (Ukawa), kiasi kwamba kila tukio lake lilikuwa likikusanya umati mkubwa, kama vile alipokwenda kuchukua fomu za urais na mkutano wa uzinduzi wa kampeni hivi karibuni jijini Dar.
Lakini baada ya Slaa kujitokeza na kueleza sababu hasa zilizomfanya ajiweke pembeni na siasa, maelfu ya wafuasi wa Ukawa Tanzania nzima wamejikuta wakisita hasa kutokana na ukweli kuwa hadi sasa, viongozi wa Ukawa na Lowassa wameshindwa kujibu hoja hata moja juu ya madai yake yaliyoibua upya mjadala wa mustakabali wa upinzani nchini.
Hali hiyo inathibitishwa na kujiengua kutoka Chadema kwa wafuasi wengi wa chama hicho, ikiwa ni pamoja na hofu ya viongozi hao kufuatia tetesi kuwa Slaa ana mpango wa kuzunguka nchi nzima kuwaaga Watanzania ambao aliwafanyia kazi kwa takriban miaka 20.
“Viongozi wa Ukawa wameshindwa kujibu hoja juu ya ufisadi wa Lowassa katika sakata la Richmond, hata ukimya wake, kunawapa watu hisia kuwa kilichosemwa na Slaa kwa miaka yote ni sahihi,” alisema kada wa Chadema, aliyejitambulisha kwa jina la Amos Mallya, ambaye aliweka wazi kuwa yeye atamfuata Slaa.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.