Hamida Hassan
Kwa mifano hiyo ya wasanii hao ambao leo hii hawasikiki kutokana na kujihusisha na kampeni za kisiasa eti iwe fundisho kwa mastaa wa sasa ambao wamejianika kuwa ni wafuasi wa vyama f’lani vya siasa.
Watu hao wanataka kutuaminisha kwamba, staa akijitangaza tu kwamba yeye ni Ukawa au CCM na akakipigia kampeni chama chake kuhakikisha kinaishika dola, anajishusha kisanii na hata baada ya uchaguzi hawezi kubaki kwenye soko.
Tuamini hivyo?
Bado sijaelewa vizuri kwamba wanaotoa hoja hizo wanasimamia wapi kwa sababu, ninachojua kila mtu ana haki ya kuwa mwanachama wa chama anachokiamini, awe ni msanii au mwananchi wa kawaida.
Sasa kuna shida gani Wema Sepetu ambaye ni staa mkubwa hapa nchini kuwa CCM na Jacqueline Wolper kuwa Ukawa? Tatizo liko wapi? Hivi hoja iko wapi ya kwamba Wema akiipigia debe CCM atapoteza mashabiki wa kazi zake?
Nauliza hivyo kwa kuwa siamini kama yupo shabiki wa kumchukia Wolper na asinunue kazi zake kwa kuwa tu ameamua kuwa Ukawa. Sidhani kama yupo mtu wa aina hiyo na kama yupo atakuwa na matatizo.
Ndiyo maana sioni dhambi ya wasanii kushabikia na kupigia debe vyama wanavyoamini kwamba vitaleta mabadiliko.
Wapo wasanii ambao wamekuwa kimya kwenye suala la siasa hasa katika kipindi hiki ambacho ni ishu. Wengine wamefikia hatua ya kusema eti hawana vyama lakini ukifuatilia utagundua kuwa wamejiandikisha kwa ajili ya kupiga kura ifikapo Oktoba 25, mwaka huu.
Kauli ya kwamba ‘sina chama’ inatolewa na msanii mkubwa ambaye nyuma yake kuna watu wanamuamini, eti kwa sababu tu akisema yeye ni CCM anahisi mashabiki wake ambao wako Ukawa watamchukia, hii inakuja kweli?
Mwanadada ambaye ni msanii na mwanamitindo maarufu, Jokate Mwegelo ‘Kidot’ aliwahi kuulizwa yeye yuko upande gani, akadai eti hana chama. Elizabeth Michael naye juzikati akajitokeza na kusema hivyo hivyo, so what?
Tumeshaambiwa msanii ni kioo cha jamii, sasa kama wewe msanii mwenye watu wengi nyuma unasema huna chama, unataka na wale walio nyuma yako wafanyeje? Hatari iko wapi ya wewe kusema uko CCM au Ukawa ili wanaokuamini wakufuate? Hii ni hofu ya kijinga!
Tujifunze kwa wenzetu
Kama wewe ni mfuatiliaji wa siasa za kimataifa, utakumbuka kuwa kipindi cha uchaguzi kule Marekani mwaka 2012 vyama vikuu, Democrat na Republican vilikuwa vikichuana ile mbaya.
Wasanii wakubwa wakagawanyika, wapo waliojitokeza na kumuunga mkono Barack Obama kama vile Jay Z, Beyonce, Kanye West na wengineo. Wakiwa wafuasi wa Democrat wakamfanyia kampeni hadi wakamuingiza Ikulu akimuangusha mwenzake wa Republican, Mitt Romney. Je, wale walipotea kisanii? Siasa imeathiri maisha yao ya kimuziki? Wala haikuwa hivyo!
Sasa wewe msanii mwenye nguvu na unayejiamini kwa kazi yako unashindwa nini kuwa na upande na ukatumia nguvu yako kuhakikisha unamuingiza Ikulu yule unayependa?
Kumbuka, kupotea kwako kwenye soko kutatokana na ubora wa kazi zako. Kama utatoa wimbo mzuri, hata kama uko Ukawa watu wa CCM watanunua. Kama uko CCM na ukatoa filamu kali, niamini mimi hata watu wa Ukawa watanunua na utazidi ‘kushaini’. Elewa kwamba kipindi hiki cha siasa ni cha mpito, tutafanya kampeni kuhakikisha vyama tunavyovishadadia vinashinda lakini hata vikishindwa, maisha yetu ya kisanii yatakuwa vilevile
Wakati f’lani
nilipata kusikia watu wakisema kuwa mwanamuziki au muigizaji kujihusisha
na masuala ya siasa ni kujipoteza kwenye ramani ya fani anayoitegemea
kuendesha maisha yake.
Watu hao wakatolea mifano ya baadhi ya wasanii ambao siwezi kuwataja hapa kwamba, miaka ya nyuma walikuwa wakila shavu kwenye kampeni za kisasa lakini baada ya uchaguzi wakapotea na sasa yamebaki majina yao tu. Kwa mifano hiyo ya wasanii hao ambao leo hii hawasikiki kutokana na kujihusisha na kampeni za kisiasa eti iwe fundisho kwa mastaa wa sasa ambao wamejianika kuwa ni wafuasi wa vyama f’lani vya siasa.
Watu hao wanataka kutuaminisha kwamba, staa akijitangaza tu kwamba yeye ni Ukawa au CCM na akakipigia kampeni chama chake kuhakikisha kinaishika dola, anajishusha kisanii na hata baada ya uchaguzi hawezi kubaki kwenye soko.
Tuamini hivyo?
Bado sijaelewa vizuri kwamba wanaotoa hoja hizo wanasimamia wapi kwa sababu, ninachojua kila mtu ana haki ya kuwa mwanachama wa chama anachokiamini, awe ni msanii au mwananchi wa kawaida.
Sasa kuna shida gani Wema Sepetu ambaye ni staa mkubwa hapa nchini kuwa CCM na Jacqueline Wolper kuwa Ukawa? Tatizo liko wapi? Hivi hoja iko wapi ya kwamba Wema akiipigia debe CCM atapoteza mashabiki wa kazi zake?
Nauliza hivyo kwa kuwa siamini kama yupo shabiki wa kumchukia Wolper na asinunue kazi zake kwa kuwa tu ameamua kuwa Ukawa. Sidhani kama yupo mtu wa aina hiyo na kama yupo atakuwa na matatizo.
Ndiyo maana sioni dhambi ya wasanii kushabikia na kupigia debe vyama wanavyoamini kwamba vitaleta mabadiliko.
Wapo wasanii ambao wamekuwa kimya kwenye suala la siasa hasa katika kipindi hiki ambacho ni ishu. Wengine wamefikia hatua ya kusema eti hawana vyama lakini ukifuatilia utagundua kuwa wamejiandikisha kwa ajili ya kupiga kura ifikapo Oktoba 25, mwaka huu.
Kauli ya kwamba ‘sina chama’ inatolewa na msanii mkubwa ambaye nyuma yake kuna watu wanamuamini, eti kwa sababu tu akisema yeye ni CCM anahisi mashabiki wake ambao wako Ukawa watamchukia, hii inakuja kweli?
Mwanadada ambaye ni msanii na mwanamitindo maarufu, Jokate Mwegelo ‘Kidot’ aliwahi kuulizwa yeye yuko upande gani, akadai eti hana chama. Elizabeth Michael naye juzikati akajitokeza na kusema hivyo hivyo, so what?
Tumeshaambiwa msanii ni kioo cha jamii, sasa kama wewe msanii mwenye watu wengi nyuma unasema huna chama, unataka na wale walio nyuma yako wafanyeje? Hatari iko wapi ya wewe kusema uko CCM au Ukawa ili wanaokuamini wakufuate? Hii ni hofu ya kijinga!
Tujifunze kwa wenzetu
Kama wewe ni mfuatiliaji wa siasa za kimataifa, utakumbuka kuwa kipindi cha uchaguzi kule Marekani mwaka 2012 vyama vikuu, Democrat na Republican vilikuwa vikichuana ile mbaya.
Wasanii wakubwa wakagawanyika, wapo waliojitokeza na kumuunga mkono Barack Obama kama vile Jay Z, Beyonce, Kanye West na wengineo. Wakiwa wafuasi wa Democrat wakamfanyia kampeni hadi wakamuingiza Ikulu akimuangusha mwenzake wa Republican, Mitt Romney. Je, wale walipotea kisanii? Siasa imeathiri maisha yao ya kimuziki? Wala haikuwa hivyo!
Sasa wewe msanii mwenye nguvu na unayejiamini kwa kazi yako unashindwa nini kuwa na upande na ukatumia nguvu yako kuhakikisha unamuingiza Ikulu yule unayependa?
Kumbuka, kupotea kwako kwenye soko kutatokana na ubora wa kazi zako. Kama utatoa wimbo mzuri, hata kama uko Ukawa watu wa CCM watanunua. Kama uko CCM na ukatoa filamu kali, niamini mimi hata watu wa Ukawa watanunua na utazidi ‘kushaini’. Elewa kwamba kipindi hiki cha siasa ni cha mpito, tutafanya kampeni kuhakikisha vyama tunavyovishadadia vinashinda lakini hata vikishindwa, maisha yetu ya kisanii yatakuwa vilevile
Note: Only a member of this blog may post a comment.