Imelda Mtema
Mume wa Miss Tanzania 2011,
Salha Israel, Abdulatif Fundikira ‘Tiff’ ameibuka na kusema kuwa kwa
mkewe wa zamani, Jacqueline Patrick alipotea njia hivyo anashukuru Mungu
sasa amefika panapostahili.
Miss Tanzania 2011, Salha Israel
Akichonga na Ijumaa
Tiff alisema kuwa kwa mkewe Salha amefika na kutokana na huduma
anazompa amegundua kuwa mkewe wa zamani Jacqueline ambaye kwa sasa
anatumikia kifungo jela nchini China hakuwa mke bora.
Jack Cliff
“Salha ni mwanamke mwenye sifa zote,
kuna wakati najisahau kabisa kama nilipitia machungu ya ndoa kwa jinsi
anavyonijali na kunithamini kwa kiasi kikubwa. Siku zote nitajisifia
kuwa naye na nitampenda na kumthamini zaidi,” alisema Tiff.
Note: Only a member of this blog may post a comment.