Mkongomani na Mkewe.
Musa Mateja na Imelda Mtema
KIMENUKA! Siku chache
baada ya kumwanika mchumba’ke, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
ambaye tayari amemvisha pete ya uchumba, mambo yamekuwa siyo mambo kwa
staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe kutokana na mke wa
jamaa huyo kuibuka na kumtaka amwachie mumewe.
Mkongomani na Wolper.
Chanzo makini kimelieleza Ijumaa Wikienda
kwamba, baada ya habari na picha za Wolper na Mkongomani huyo
kuripotiwa na gazeti ndugu na hili, Risasi Jumamosi, mke wa ndoa wa
mwanaume huyo alijitokeza na kuvunja ukimya akimtaka mwigizaji huyo
aachane na mumewe huyo mara moja kabla hajamchukulia hatua za kisheria
kwa sababu ameingilia ndoa yake.
“Unajua baada ya ninyi (Global) kuanika
picha za Wolper kwenye gazeti na mitandao mbalimbali ya kijamii
akivishwa pete ya uchumba na Mkongomani, mke wake ameshindwa kuvumilia
hivyo amelazimika kumtumia ujumbe Wolper akimtaka aachane na mume wake
kwani kama alikuwa hana taarifa kuanzia leo (Jumamosi) atambue kwamba
huyo mwanaume ni mume halali wa mtu na ana watoto ndani ya ndoa.
“Yaani mke wa Mkongomani amemjia juu
Wolper akimtaka amwachie mumewe, ajiweke pembeni mara moja na kama
alidanganywa kuwa huyo mwanaume hajaoa, basi atambue kwamba tayari
alishafunga naye pingu za maisha, tena kanisani na tayari ana familia ya
watoto wawili, haoni sababu ya kumnyamazia maana ameumia sana hivyo
anamtahadharisha ili baadaye asije akaanza kulia akisema hajaambiwa,”
kilisema chanzo hicho.
MSIKIE WOLPER
Ili kuweka mzani wa habari hiyo, Ijumaa Wikienda
lilimtafuta Wolper ili kujua kama ameshayapata malalamiko hayo ambapo
alifunguka kuwa, kuna maneno mengi yanazungumzwa juu ya tukio hilo
lakini ukweli wa mambo zaidi anaufahamu yeye na mchumba’ke huyo hivyo
haoni sababu ya kumwambia kila mtu maana mpaka anafikia uamuzi wa
kuvishwa pete tayari walishajadiliana vya kutosha.
“Naweza kusema kwamba ni moja ya
historia katika maisha ya mchumba wangu hivyo hata nilipoona hizo picha
za mkewe hakuna jambo lililonishtusha kwani tayari alikuwa ameshaniambia
juu ya misukosuko aliyoipitia kwenye ndoa yake huko nyuma.
“Hadi anafikia hatua ya kunivisha pete
basi watu wanatakiwa kujua tu kwamba kila jambo liko sawa na zaidi wao
wanatakiwa kusubiri hadi siku ya ndoa yetu waone kama itafungwa au lah.
“Siku hizi dunia imekuwa kama kijiji
hivyo huwezi kuwazuia watu kuongea jambo, mchumba wangu ananijua na mimi
ninamjua kwa kina, pamoja na kwamba watu pia wamekuwa wakimletea maneno
kuhusu mimi lakini nimemwambia aachane nao kwani hakuna sababu ya
kujibizana nao, kwa sababu kila mtu ana uhuru wa kutumia kinywa chake
jinsi anavyoweza maana ningekuwa sijui background (maisha ya nyuma) yake
kweli baada ya kuona hizo picha za mkewe na maneno ya watu wanayosema
ingeniuma sana.
“Nafikiri watu wanachotakiwa kujua juu
yetu ni kwamba Mungu akishapanga jambo kamwe binadamu hawezi kulipangua
hata iweje na kwa maana hiyo sasa hata mwanaume akishakupenda ni ngumu
kumsikiliza mtu mwingine maana upendo wa mtu ni moyo na nafsi yake
mwenyewe ndiyo inayoweza kumuongoza kwa kila hali.
“Watu wameshafanya kila juhudi za
kutugombanisha lakini sasa ameshazoea hadi anavichukulia kama burudani
tu, hata mimi haya ninayaona kama matangazo ya biashara hivyo hakuna
linaloniumiza kichwa,” alisema Wolper.
ETI ANA GUNDU?
Kutokana na kitendo hicho wadau
mbalimbali walifika mbali na kudai kwamba mwanadada huyo inawezekana ana
gundu kwani ameshakuwa na wanaume tofauti na wengine kumvisha pete ya
uchumnba na kutambulishana kwa wazazi lakini ikawa ndivyo sivyo.
“Wolper anatakiwa kujiangalia sana na
kumuomba Mungu kwani siyo mara ya kwanza kuwa na wanaume wa watu,
kinachowaponza hawa mastaa wetu wana tamaa sana ya fedha ambazo
huwasababisha kuwa na mtu kwenye uhusiano bila kumchunguza vizuri,”
alisema mdau mmoja mkazi wa Mwenge, Dar.
TUJIKUMBUSHE
Kwa Wolper, kuvishwa pete ya uchumba
siyo mara ya kwanza kwani awali aliwahi kuvishwa na aliyekuwa mpenzi
wake, Abdallah Mtoro ‘Dallas’ lakini hawakufikia hatua ya kufunga ndoa
wakaachana solemba.

Note: Only a member of this blog may post a comment.