Gladness Mallya MWANADADA
anayefanya vizuri kwenye tasnia ya filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’
ameibuka na kusema hawezi kumrudia aliyekuwa mpenzi wake, msanii
Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
Salma Jabu ‘Nisha’.
Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki, Nisha alisema
amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya kuenea kwa uvumi kuwa ana
mpango wa kurudiana naye, jambo alilosema haliwezekani kwani kwake hana
tabia ya kula matapishi.
“Siwezi kurudiana na Nay, kwanza ana mwanamke mwingine na kuzaa naye
japo wameachana, mwanzo nilimuogopa sana nikimuona, lakini hivi sasa
nimeshamzoea, tumebaki kama kaka na dada, suala la mapenzi haliwezi
kujirudia tena,” alisema.

Note: Only a member of this blog may post a comment.