Byser amesema kuwa wimbo wake mpya ‘Baki na Mimi’, unagusa moja kwa moja maisha yake na mke wake Warda.
“Wimbo huu unagusa maisha ya mimi na mke wangu Warda kwa asilimia kubwa, wengi hawajui kuwa mke wangu nilikutana naye club, mazingira ambayo wengi wanadhani si mazuri kwa mwanamke, lakini kwangu ni tofauti kwa kuwa mke wangu ana sifa zote za kuwa mke,” alisema Blue.
Mr Blue na mke wake wamepata mtoto wa pili wa kike wiki iliyopita. Wamempa jina la Khairriyah.
Chanzo: Mtanzania

Note: Only a member of this blog may post a comment.