Mgombea
wa Ukawa aliyeteuliwa kuwania Ubunge wa Jimbo la Nzega Mjini kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Charles Mabula (kulia)
akipeana mkono na aliyekuwa Mgombea wa nafasi hiyo kwa Jimbo la Nzega
mjini, Mezza Leonard (kati) aliyekubali kushindwa baada ya kupigwa kura
ya wazi na wananchi wa Nzega Mjini, Septemba 6, 2015. Kushoto ni
Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amesema ili umasikini unaowakabili Watanzania uweze kuondoka lazima washirikiane kuiondoa madarakani CCM.
Amesema ulofa na upumbavu wanaodaiwa kuwa nao Watanzania umesababishwa na Serikali ya CCM kwa kuwa haiwajali Watanzania.
Mbowe alitoa kauli hiyo jana alipohutubia mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Laini Polisi mjini Nzega, Mkoa wa Tabora ambapo pia alilazimika kuwapigisha kura za mikono wananchi wa Nzega waliohudhuria mkutano huo ili kutatua mvutano wa wagombea wa ubunge katika Jimbo la Nzega Mjini lililokuwa na wagombea wawili wa Ukawa.
Wakati wa kura hizo, mgombea wa Chadema, Charles Mabura, aliibuka mshindi dhidi ya mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Meza John


Note: Only a member of this blog may post a comment.