Brighton Masalu
MASKINI! Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma amezimia ndani ya
gari, kisa kikiwa ni sakata la dada zake kuibiana mume, Amani linaweza
kuandika.
Mkasa huo wa kusikitisha ulijiri mapema wiki hii, Kinondoni, Dar
ambapo staa huyo alikuwa ameegesha gari lake pembeni mwa barabara.
Kabla ya kuzimia, Wastara aliliambia Amani kuwa, kitendo cha mdogo
wao (mtoto wa mama yao mdogo), Janat kupora mume wa dada yake, Naima
Juma (dada wa damu wa Wastara) aitwaye Masoud na kufunga naye ndoa
kimyakimya, kimeipasua familia.
Wakati mahojiano yakiendelea, ghafla Wastara alianza kuangua kilio na kulaani kitendo hicho akikiita cha kinyama.
“Kinachoniuma ni kitendo cha mama wa Janat, Jamila Salum kutamka kuwa
lazima mwanaye aoelewe na Masoud ambaye ni shemeji yake kwa Naima, kama
ni kuvunjika kwa undugu, iwe hivyo.
“Nilimtegemea kwa ushauri na malezi bora lakini kitendo cha binti
yake kuchukua mume wa dada yake, naye kuunga mkono ni aibu,” alisema
Wastara.
Baada ya kama dakikia 15, Wastara alizinduka na muda mfupi baadaye
alisema safari hii hatakubali kuona dada yake akiporwa mume huku ndugu
zao wakichekelea na kwamba kama ‘mbwai mbwai tu’.
Note: Only a member of this blog may post a comment.