Thursday, September 10, 2015

Anonymous

Majibu ya GWAJIMA Kwa Dk. SLAA Yaibua Mazito!

Mchungaji wa Kanisa la Huduma ya Ufufuo na Uzima lenye makao yake makuu jijini Dar, Josephat Gwajima.
NI mwaga ugali, mimi nimwage mboga! Ndivyo inavyoonekana katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu nchini kote.
Hali hiyo inafuatia Mchungaji wa Kanisa la Huduma ya Ufufuo na Uzima lenye makao yake makuu jijini Dar, Josephat Gwajima kuibuka juzi na kujibu mapigo ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, baadhi ya waumini, hasa wa Kikristo wamekuwa kinyume.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa.
Wakizungumza na gazeti hili baada ya Gwajima kumaliza hotuba yake aliyoitoa kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Landmark jijini Dar, walionesha wasiwasi kwa mtumishi huyo wa Mungu kuanika siri za maisha ya ndoa ya muumini wake.

“Gwajima alijitetea vizuri lakini mimi nimetatizika na kumchambua Slaa na mkewe. Alisema Slaa alikuwa akimpigia simu wakati mkewe (Josephine Mushumbusi) amepandisha mapepo. Mimi naamini Slaa alifanya vile kwa sababu yeye ni mtumishi wa Mungu, alijua siri ya mapepo ya mkewe yatasitiriwa, sasa kusema hadharani sidhani kama ni sahihi,” alisema Grace Miriam, mkazi wa Mwenge, Dar.

Mwingine alisema: “Mimi ni muumini wa kanisani kwa Gwajima. Sitaki kutaja jina. Lakini kitendo cha kufukunyua maisha ya muumini mwingine mbele za watu kinanipa wasiwasi. Mimi nina ndoa, kumbe nikisema nipeleke matatizo yangu kwake, ipo siku atanianika, si ndiyo!”

Wengi walisema Gwajima alikwenda kinyume na viapo vya utumishi wa Mungu, kutotunza siri ya muumini. Walisema mchungaji ni kama daktari asivyotakiwa kutoa siri ya mgonjwa.

Hata hivyo, katika mkutano huo, Gwajima alijitetea kwamba alitaka kumjibu Slaa kufuatia mkutano wake na wanahabari hivi karibuni katika Hoteli ya Serena, Dar akisema, mtumishi huyo ni mshenga kwa vile ndiye aliyesimamia zoezi la waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuhamia Chadema madai aliyosema si ya kweli ila Dk. Slaa alitakiwa na mkewe kuachana na siasa.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.