Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiweka udongo katika kaburi la marehemu Kombani.
Spika wa Bunge, Anne Makinda akiweka udongo katika kaburi la marehemu Celina Kombani. Nyuma yake ni Samia Suluhu.
Mama Salma Kikwete naye akiweka udongo kwenye kaburi la Kombani.
Bwana Hemed Saleh Pongoleni ambaye ni mume wa marehemu akiweka shada la maua katika kaburi la mke wake, Celina Kombani.
Watoto wa marehemu wakiwa na mashada ya maua wakati wa maziko ya mama yao.
Viongozi mbalimbali wakishiriki maziko hayo.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Celina Kombani likiingizwa kaburini.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa
heshima zake za mwisho mbele ya mwili wa Waziri Celina Kombani katika
Uwanja wa Jamhuri, mkoani Morogoro.
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akiaga mwili wa Waziri Kombani leo.
Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda
akitoa heshima zake mbele ya jeneza lenye mwili wa Waziri Celina
Kombani kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
IGP Mstaafu, Omar Mahita naye akitoa heshima zake za mwisho.
Baadhi ya wasanii wakitoa heshima zao za mwisho.
MAKAMU wa Rais, Dk. Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda
leo wameongoza mamia ya waombolezaji katika maziko ya aliyekuwa Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani
yaliyofanyika kwenye shamba lake lililopo Lukombe nje kidogo ya Mji wa
Morogoro.
Kombani ambaye alikuwa mbunge wa Jimbo la Ulanga Mashariki alifariki
dunia Alhamisi iliyopita katika Hospitali ya Andhraprasth Appollo ya
mjini Delhi, India alikokuwa amelazwa akitibiwa saratani ya kongosho.
Viongozi wengine walioshiriki maziko ya Mhe. Kombani ni pamoja na Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete, Spika wa Bunge Anne Makinda, Mgombea Mwenza
wa urais kupitia CCM Samia Suluhu, IGP Mstaafu Omar Mahita na wengineo.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Celina Kombani mahali pema peponi. AMEN.
(PICHA ZOTE NA DUNSTAN SHEKIDELE / GPL, MOROGORO)
Note: Only a member of this blog may post a comment.