Mafuriko ya wananchi katika Kijiji cha Mvumi, Jimbo la Mtera yakimsiliza Magufuli alipokuwa akimwaga sera.
Magufuli akibadilisha mawazo na mgombea Ubunge wa jimbo la Isimani, William Lukuvi.
Magufuli akiongea na wakazi wa kijiji cha Pawaga.
Mgombea ubunge wa jimbo la Isimani William Lukuvi akiongea na wakazi wa Kijiji cha Pawaga jimbo la Isimani, Iringa.
Mzee John Malechela alitumia zaidi ya dakika 20 kuwaeleza umuhimu wa kumchagua magufuli kwa ajili ya maendeleo ya taifa hili
RPC wa
Iringa, Ramadhan Mungi akiongea na wanahabari juu ya watu waliofanya
vurugu mjini iringa jana, ambapo watu 62 akiwemo Mgombea Ubunge kupitia
RPC wa
Iringa, Ramadhan Mungi akiongea na wanahabari juu ya watu waliofanya
vurugu mjini iringa jana, ambapo watu 62 akiwemo Mgombea Ubunge
kupitia[1]
Umati mkubwa ulijitokeza kwenye viwanja vya shule ya msingi mvumi ukiwa tayari kusikiliza sera za magufuli
Wakazi wa kijiji cha Chipogoro, Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wakiwa kwenye shamrashamra za kumpokea Magufuli
Wakazi wa kijiji cha Chipogoro, Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wakiwa kwenye shamrashamra za kumpokea Magufuli.
Wakazi wa kijiji cha Pawaga Jimbo la Isimani, wakiwa tayari kumsiliza Magufuli
Mgombea urais wa CCM, John Magufuli, leo
alimalizia kampeni yake mkoani Iringa kwa kufanya mkutano uliohudhuliwa
na umati mkubwa katika Kijiji cha Pawaga Jimbo la Isimani mkoani hapo.
Baada ya mkutano huo uliohudhiliwa na maelfu ya
wakazi wa kijiji hicho na vijiji jirani Magufuli alimwaga sera na kisha
kuomba kura kwa wakazi hao. Baada ya kutoka kijiji hicho Magufuli
alisonga mpaka mkoani Dodoma na kupokelewa na maelfu ya wananchi
waliokuwa wakimsubili katika Kijiji cha Migori Jimbo la Kibakwe ambapo
wakazi hao walionesha furaha na matumaini baada ya Magufuli kuwaahidi
serikali yake kutoa elimu bure elimu bure kuanzia darasa la kwanza mpaka
kidato cha nne pamoja na kuwaboreshea barabara zinazoingia na kutokea
kijijini hapo. Kwa leo Mafuguli alimazia kampeni zake katika Kijiji cha
Mvumi ambapo Magufuli alipokelewa na mafuriko ya wakazi wa kijijini hapo
walioongozwa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtera Livingstone Lusinde na
Makamu wa Rais Mstaafu, John Malechela. Kampeni hizo zinatarajia
kuendelea kesho mkoani Dodoma.
HABARI/ PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL
Note: Only a member of this blog may post a comment.