Wasanii wengi wa Bongo wamesitisha kutoa kazi zao katika kipindi hiki
cha uchaguzi kwa kuhofia kuzipoteza kwa kumezwa na kampeni za siasa,
lakini Belle 9 aliamua kujitosa na kutoa video yake mpya ‘Shauri Zao’
wiki iliyopita.
Belle 9 ameiambia Bongo 5 kuwa hajutii kutoa video katika kipindi
hiki kwasababu kutokana na wasanii wengi kuogopa kutoa kazi zao imefanya
apate nafasi ya kazi yake kuonekana zaidi ya alivyotarajia.
“Hakuna msanii ambaye kaachia video sasa hivi ambayo ina tension kama
mimi” amesema Belle 9. “pia kati ya vitu ambavyo vinaongelewa
ukiongelea watu watatu ambao wanakick nipo na mimi kwa sasa hivi,
ukiingia kwenye mitandao watu ambao habari zetu zipo sana saizi. Naona
uwanja umekuwa wangu peke yangu sana, kuna matokeo mazuri zaidi ya
nilivyokuwa nategemea.”
Belle ameongeza kuwa video ya ‘Shauri Zao’ niliyokuwekea hapo chini ndio video yake bora kati
ya video zake zote alizofanya kutokana na umakini wake na wa director
Hanscana aliyeifanya.
Note: Only a member of this blog may post a comment.