Wednesday, September 23, 2015

Anonymous

MADAI MAZITO: Ukaribu wa Mkurugenzi wa TWAWEZA na MAKAMBA wa CCM Waibua Mapya!

Aidani Eyakuze ni Mkurugenzi mkuu wa Tweweza east africa, namfahamu sana kijana huyu aliyechukua nafasi ya Rakesh pale Twaweza. Eyakuze ni rafiki mno tena wa karibu sana na January Makamba, na katika ile proposal concept ya Makamba pale Mlimana city ya kutangaza nia pale mlimani Eyakuze ndiye aliyekuwa consultant mkuu wa ile proposal ambayo leo kwa kiasi kikubwa imekuwa updated na Mgombea wa CCM Magufuli na Makamba kuwa karibu kuhakikisha inatekelezeka mfano kuipa kila kijiji sh milioni 50.

BADO naconnect urafiki wa Eyakuze na Makamba katika takwimu alizozitoa Juzi ktk media January na leo za Twaweza....Ni kama watu wanalala na kuamka pamoja.

Kwa thread hii, Aidani Eyakuze ameidhalilisha taasisi kubwa kama Twaweza kwa kununuliwa na CCM kupitia January na kupika tafiti zenye kuifurahisha CCM...hii ni hatari sana kwa taaluma ya Aidan Eyakuze ambaye Taasisi yake inaheshimika kwa tafiti zenye kulenga kuboresha mambo mbali mbali kwa serikali kwa watu wake. Mfano mmoja ni Elimu kwa kupitia mradi wake wa UWEZO Tanzania inafanya tafiti na kuipa mrejesho serikali kwa changamoto mbali mbali za ukweli toka kote nchini na serikali kupitia wizara ya elimu na TAMISEMI mara nyingi imeonyesha mabadiliko na kufanya utekelezaji kwa baadhi ya maeneo hayo Muhmu. sasa My take ....kama CCM inakununua Aidan..Hivi chama hiki kikiwa madarakani kiendelee kuamini na kufanyia kazi tafiti zako zijazo? Na hasa sasa nasikia mtaongeza evaluation katika afya na mazingira?

Aidani sio masikini wa hela kwa elimu na nafasi yake pale Twaweza...Uswahiba wake tena wa siku nyingi na January anaamua kupindisha taaluma yake na taasisi yake kutoa matokeo ya kufurahisha CCM hii haitoshi kuzuia maamuzi ya wananchi wanaotaka mabadiliko ambayo UWEZO Tanzania imevumbua madudu mengi tu uko chini katika tafiti zake za elimu kwa miaka 5 mfululizo. Aidan wanishangaza sana.


IMAGE ya Twaweza na UWEZO Kenya, Uganda na Tanzania inaenda kuingia doa na dosari kubwa sana kwa upenzi huu binafsi wa Aidan Eyakuze na January Makamba.

Hivi dhambi hii kwa CCM, January na Aidan mtaungamia wapi ili hali nafsi zenu zinajua mnafanya hujuma ya makusudi.....shame on YOU Aidan na Shame on Makamba.

Mungu akupe uhai mrefu Mr Rakesh, hata kama Mkapa alikuwa rafiki yako sana ulimkosoa sana na kumpa fact wakati wa "HAKI ELIMU" hadi ulipoingia TWAWEZA hukusita kufanya hivyo kwa Kikwete na mengi tumeyaoona yanabadilika.....lakini kwa aliyechukua Kijiti chako Aidan Eyakuze huku sio tena ameendeleza ameamua kufanya Twaweza na UWEZO kuwa taasisi Ndogo za CCM. Shame na kwa washauri wake Uganda, Tanzania, na Kenya..
Source: Jamii Forums

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.