Ijumaa September 11 2015 imeanza na uchambuzi wa magazeti redioni @CloudsFM, kama hukuweza kusikiliza uchambuzi wa magazeti asubuhi hii karibu uzipate zile kubwa za leo hapa chini…
BAKWATA yampitisha Sheikh Abubakar Muzeri kuwa Mufti wa Tanzania, Rais Jakaya Kikwete jana alipokea tuzo nyingine ya uongozi bora barani Africa kwa mwaka 2015 nchini Africa Kusini.
Mbungue wa CCM Nkasi kaskazini Ally Kessy aibuka kwenye mkutano wa ACT Wazalendo na kupinga maelezo juu ya mshahara wake, mgombea Urais kupitia CCM John Magufuli awaombwa wananchi mkoani Mara wasikiadhibu Chama hicho.
Steven Wasira amekana kutoa rushwa, Mgombea Urais kupitia CHADEMA Edward Lowassa awataka CCM kuacha uongo, Tundu Lissu aichana Serikali, Uchaguzi Mkuu 2015 wavutia waangalizi 400 mpaka 600 kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Nyingine kwenye magazeti asubuhi hii,
Mwalimu aongezewa mshahara kwenye makaratasi tu lakini hakuna hela
iliyoingia toka apande madaraja mawili na wagonjwa 989 walazwa kwa Kipindupindu jijini Dar es salaam .
Sauti ya uchambuzi wote asubuhi hii kwenye #PowerBreakfast nimeirekodi na kukuwekea hapa chini.

Note: Only a member of this blog may post a comment.