Saturday, September 5, 2015

Anonymous

LIVE! JOKATE KIDOTI, KIBA WAJIANIKA KIMAHABA!

Musa mateja
POTELEA mbali! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia wapendanao, mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na staa wa Bongo Fleva, Ali Kiba ‘King Kiba’ kuamua kujilipua kwa kuanika hadharani picha zao za kimahaba licha ya wazazi wa mrembo huyo kutobariki uhusiano huo kwa kigezo cha kutofautiana dini, Risasi Jumamosi linakupa mchapo kamili.

Hivi karibuni, ilidaiwa kuwa Jokate alimtambulisha nyumbani kwao lakini wazazi wake walimchomolea kwa madai kuwa hawaendani kiimani.Jumanne iliyopita, chanzo chetu kilimtonya paparazi wetu kuwa Jokate ametupia picha hiyo katika akaunti yake ya mtandao wa Instagram ndipo ‘fasta’ mwanahabari wetu aliposhughulikia ubuyu huo.

“Ametupia sasa hivi, ingia fasta katika akaunti yake utaona. Inaonesha kabisa wapo pamoja usiku huu na si ajabu watakuwa nyumbani kwa Kiba Upanga maana kuna mtu aliniambia huwa mara kadhaa wanalala mpaka asubuhi,” kilipenyeza chanzo hicho.

Baada ya kuingia kwenye ukurasa huo, mwanahabari wetu aliiona picha hiyo iliyomuonesha Jokate akimbusu Kiba kimahaba hivyo kutoa tafsiri kwamba bado wanaendeleza safari yao ya ‘kimalovee’.Saa chache mbele baada ya kuiweka picha hiyo, mrembo huyo aliitoa hususan baada ya wadau mbalimbali kuanza kumpongeza kwani wamekuwa wakifanya siri sana kuanika penzi lao.

Mwanahabari wetu alipomtafuta Jokate ili kujua sababu za yeye kuweka na kuitoa picha hiyo katika akaunti yake, kama kawaida yake, simu yake iliita bila majibu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, hakujibu chochote.
Kama ilivyokuwa kwa Jokate, alipotafutwa Kiba naye hakutoa ushirikiano.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.