Friday, September 11, 2015

Anonymous

Kocha TAIFA STARS Afichua Siri ya Wachezaji wa SIMBA SC

KIBADENINEWQW
Wilbert Molandi, Dar es Salaam
MSHAURI wa Benchi la Ufundi la Taifa Stars, Abdallah Kibadeni ambaye kitaaluma ni kocha, ametaja sababu ya wachezaji wa Klabu ya Simba kutopata nafasi kubwa katika kikosi cha kwanza cha Stars katika mechi dhidi ya Nigeria.
Kibadeni amejitokeza kufunguka juu ya suala hilo ambalo limekuwa likizungumzwa mitaani kutokana na kikosi cha Stars kukosa mchezaji wa Simba katika 11 walioanza kwenye mchezo huo wa Jumamosi iliyopita.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Kibadeni alisema hawakupanga kikosi kwa kuangalia majina ya timu, bali uwezo wa mchezaji na aina ya mbinu walizozipanga.
“Tulitumia akili ya kisayansi kukipanga kikosi hicho kutokana na kutojua falsafa na mbinu za kocha mkuu mpya wa Nigeria, Sunday Oliseh. Tuliamua kuwapanga kutokana na jinsi walivyozoeana kwa muda mrefu, mfano Barthez (Ally Mustapha), Cannavaro (Nadir Haroub), Yondani (Kelvin) na Haji Mwinyi wamekuwa wakicheza pamoja na kwa kuelewana.

“Viungo Himid (Mao), Mudathir (Yahya), Farid (Mussa) na beki wa pembeni Kapombe (Shomari) nao wamekuwa na maelewano mazuri kuanzia ngazi ya klabu na hata tulivyokuwa kambini.
“Katika safu ya ushambuliaji Samatta (Mbwana), Ulimwengu (Thomas) wote wapo TP Mazembe wanajuana vizuri. Tulimuongeza Ngassa (Mrisho) kwa kuwa ni mzoefu na uwezo wake unajulikana.

“Hivyo hakukuwa na lengo baya kwa wachezaji wa Simba na wala hawatakiwi kulalamika, ndiyo maana uliona alivyoingia Ndemla (Said) naye alicheza vizuri kwa kuwa alikuwa ameshausoma mchezo. Tuache lawana na tuwapongeze vijana kwa kazi nzuri,” alisema Kibadeni.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.