Friday, September 11, 2015

Anonymous

VIGOGO Wavamia Kambi ya SIMBA SC, Waongeza Dawa

aveva
Mwandishi Wetu, Zanzibar
WAKATI Simba ikijiandaa kufungua pazia la Ligi Kuu Bara kwa kukipiga na African Sports kesho Jumamosi, vigogo wazito wa Simba, jana walivamia kambi ya timu yao muda mfupi kabla ya kupanda ndege kwenda Tanga.
Simba itakipiga na timu hiyo ya Tanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani ambapo ilipata ugeni huo ukiongozwa na Rais wa Simba, Evans Aveva ambaye alisema kuwa sababu ya kufika kambini hapo ni kuhamasisha wachezaji na benchi la ufundi kuelekea kuanza kwa msimu huo.

“Nimeambatana na viongozi wengine wa klabu yetu kwa ajili ya kuongea na ninyi, pia kuwatakia fanaka katika msimu huu mpya, sote kwa pamoja tuna imani sana na kikosi chetu hiki cha mwaka huu tumefanya usajili mzuri, timu ipo chini ya bechi la ufundi lenye weledi wa hali ya juu na hata hali ya kambi yetu kwa muda wote takriban miezi mitatu imekuwa tulivu na amani.

“Tunakwenda kupambana na kama mnavyojua wapenzi na wanachama wa Simba tunategemea ushindi mkubwa msimu huu, hivyo lazima tupambane kwa hali na mali kucheza soka la hali ya juu,” alisema Aveva.

Akizungumzia ugeni huo, nahodha wa Simba, Musa Hassan Mgosi, alisema: “Tumefarijika sana kuona viongozi wetu wamekutana na sisi, tunawaahidi wapenzi wa Simba kuwa kikosi kipo tayari kwa ajili ya mechi ya ufunguzi na ligi nzima kwa jumla, mwaka huu ubingwa ni wetu.”

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.