Imelda Mtema
AHADI ni deni! Njemba mmoja mkazi wa Mbezi Manyema,
jijini Dar aliyejulikana kwa jina la Omar Msambaa, hivi karibuni
alijikuta akipakwa lipstick, kunyolewa nywele na baadaye kuogeshwa kwa
soda aina ya mirinda, ikiwa ni kutimiza ahadi yake ya awali kuwa
afanyiwe hivyo endapo timu aliyokuwa akiishabikia itafungwa.
Njemba huyo akipakwa lipstick.
Chanzo chetu kililiambia gazeti hili kuwa, awali Msambaa, shabiki
mkubwa wa timu ya Simba, alikuwa amejiapiza afanyiwe kitendo hicho mbele
ya mjumbe wa mtaa, akitamba kuwa klabu yake haiwezi kufungwa na watoto
wadogo kama Yanga.
Baada ya ahadi hiyo, inadaiwa watu walitawanyika kila mmoja akisubiri
siku ya mchezo ifike na baada ya ‘mnyama’ kukubali kichapo cha mabao
2-0, Msambaa alitoweka eneo hilo akihofia kufanyiwa kitendo alichoahidi.
…Akinyolewa.
Inadaiwa baada ya siku kama mbili kupita, walitonywa na mtu kuwa
Msambaa alikuwa maeneo ya Tatedo, ndipo vijana wakamfuata na kumbeba
juujuu hadi kijiweni ambako walianza kutekeleza ahadi zake kwa kumnyoa
nywele, kumpaka rangi mdomoni (lipstick) na kana kwamba haitoshi,
wakamletea sufuria lililojaa maharage wakampa na mkate na kumlazimisha
kula.
Note: Only a member of this blog may post a comment.