Tuesday, September 8, 2015

Anonymous

KIMENUKA! Msemaji wa Upinzani Auawa Kinyama Burundi

11999030_980919921972002_4942488305638951283_n
Msemaji wa Chama cha Upinzani cha UPD nchini Burundi, Patrice Gahungu  ameuawa kwa kupigwa risasi katika mji mkuu wa Bujumbura.
Gahungu wa chama cha Union for Peace and Development aliuawa alipokuwa akiendesha gari kwenda nyumbani kwake siku ya jumatatu usiku.

Kiongozi wa chama hicho Zedi Feruzi naye aliuawa kwa kupigwa risasi mwezi Mei wakati wa maandamano ya kumpinga rais Pierre Nkurunziza.
Watu wengine wawili waliuliwa hapo jana mjini Bujumbura lakini polisi bado wanaendelea na uchunguzi.
Maandamano hayo yaliitishwa na upinzani kupinga hatua ya rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Watu kadha wameuawa na maelfu ya wangine wameikimbia nchi hiyo tangu kuzuka kwa mzozo mwezi Aprili.
(CHANZO: BBC SWAHILI)

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.