Baada ya urafiki wao kuyumba kwa kipindi cha zaidi ya miezi miwili
hivi iliyopita, mastaa wa Bongo Movies, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel
wameonyesha kumaliza tofauti zao na kurudisha urafiki wao kama ilivyo
kuwa awali.
Urafiki wa Wema na Aunt ulionekana kuyumba na kufikia hatua ya Wema kutohudhuria baby shower party
ya Aunt ambapo Aunt alidai kumualika Wema na hata havi karibuni aunt
alipojifungua mtoto Wema hakusema chochote kwenye ukurasa wake mtandaoni
ukizingatia kuwa wakati wa ushosti wao alikuwa na kawaidia ya kuweka
picha kadhaa za Aunt wakati anaujauzito na vile vile Wema amakuwa na
kawaida ya kuwapongeza mastaa wenzake wakijifungua kupitia ukurasa wake
huo.
Kwa kipindi cha miezi hiyo yote, wawili hawa amabo walikua mashosti
wa nguvu hawakuwahi ‘kupostiana’ kwenye kurasa zao kwenye mtandaopicha
wa Instagram tofauti na awali. Lakini jana alianza Wema kwa kuweka
picha ya Aunt kwenye ukurasa wake na kuandika mistari hii “Ka baby haka....!!! ….Mama Cookie wangu....”
Muda kidogo Aunt naye aliibuka na kuweka picha ya Wema na kuandika “Wa kwangu mm Peke yang Mtag bac Mwambie Nampenda mm apa....” Kisha akaweka picha hiyo hapo juu wakiwa wanasukana Aunt aliandika “My One an Only....Msusi wang mm no saloon “
Kwa mara nyingine wale wapambe nuksi wa Wema na Aunty ambao walikuwa
wakisigana kwenye kipindi chote hicho ambacho wawili hao walikuwa hawapo
sawa wameumbuka na kuamua kuungana na wadu wengi amabo wameonyesha
kufurahia kitendo cha mashosti hao kuwa karibu kama zamani kwa kumwaga
COMMENTS na LIKES za kutosha.
Wapambe ndiyomana mnaitwa NUKSI.
Mzee wa Ubuyu

Note: Only a member of this blog may post a comment.