Ashura Ramadhani anayedaiwa kucharangwa mapanga na mumewe.
Na Haruni Sanchawa
WIVU! Mtu mmoja
aliyejulikana kwa jina moja la Abdallah, mkazi wa Gongo la Mboto, Ilala
jijini Dar es Salaam, anadaiwa kumkatakata kwa mapanga sehemu
mbalimbali za mwili mkewe Ashura Ramadhani kwa kinachodaiwa kuwa ni wivu
wa mapenzi.
Chanzo cha kuaminika kililiambia gazeti
hili juzi kuwa Abdallah baada ya kufanya unyama huo, alikimbilia
kusikojulikana na jeshi la polisi linamtafuta ili akabiliane na sheria.
Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Gongo la
Mboto imethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo afisa mmoja alisema
wawili hao walipeleka shauri lao hapo ambapo baada ya kusikilizwa,
walikubaliana kila mmoja aishi kwenye chumba chake, uamuzi ambao hata
hivyo, mwanamke aliupinga vikali.
Ashura alipoulizwa na mwandishi wetu alikiri kutokea tukio hilo.
WIVU! Mtu mmoja
aliyeju-likana kwa jina moja la Abdallah, mkazi wa Gongo la Mboto,
Ilala jijini Dar es Salaam, anadaiwa kumkatakata kwa mapanga sehemu
mbalimbali za mwili mkewe Ashura Ramadhani kwa kinachodaiwa kuwa ni wivu
wa mapenzi.
Chanzo cha kuaminika kililiambia gazeti
hili juzi kuwa Abdallah baada ya kufanya unyama huo, alikimbilia
kusikojulikana na jeshi la polisi linamtafuta ili akabiliane na sheria.
Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Gongo la
Mboto imethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo afisa mmoja alisema
wawili hao walipeleka shauri lao hapo ambapo baada ya kusikilizwa,
walikubaliana kila mmoja aishi kwenye chumba chake, uamuzi ambao hata
hivyo, mwanamke aliupinga vikali.
Afisa huyo aliyeomba hifadhi ya jina
lake kwa kuwa siyo msemaji, alisema mwanaume alikuwa akimtuhumu mkewe
kuwa anatoka nje ya ndoa yao jambo ambalo mwanamke alilipinga. “Baada ya
wawili hao kufika nyumbani, ugomvi ulianza tena ndipo mwanaume alimkata
mkewe mapanga miguuni, kichwani na sehemu za siri,” alisema afisa huyo.
Ashura alipoulizwa na mwandishi wetu alikiri kutokea tukio hilo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.