Mkali wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Imelda Mtema
Mkali wa sinema za Kibongo,
Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kudatishwa na picha za mastaa
mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii ambao ni wajawazito kiasi ambacho
zinamuhamasisha kupata mimba.
Akizungumza na Amani,
Lulu alisema kuwa, picha za wajawazito kwa sasa zimeonekana kuwa na
mvuto kwake zaidi, jambo ambalo linamfanya apate hamasa zaidi maana
zimekuwa ndizo zenye ‘kiki’ kwa kipindi hiki.
“Picha za wajawazito kwa kipindi hiki
ndizo zimekuwa zikinipata kiki halafu ni nzuri hatari na nina hofu
zitawafanya watu wengi wapate ujauzito maana mimi mwenyewe kama zinataka
kunibadili mawazo hivi,” alisema Lulu.

Note: Only a member of this blog may post a comment.