Friday, September 18, 2015

Anonymous

Madam Rita wa BSS Awapiga Chini Wanasiasa!

madam-rita 
Jaji Mkuu wa Shindano la Bongo Star Search 2015 (BSS), Rita Paulsen ‘Madam Rita’
Na Hamida hassan
Jaji Mkuu wa Shindano la Bongo Star Search 2015 (BSS) linaloendelea hivi sasa, Rita Paulsen ‘Madam Rita’ amewapiga chini wanasiasa waliokuwa wakitamani awe nao na kusema kuwa yeye ni mfanyabiashara hivyo hawezi kusapoti chama chochote cha siasa.
madam rita2Akizungumza na Ijumaa Rita alisema kuwa kipindi hiki cha siasa amekuwa akifuatwa na wanasiasa kibao wakitaka kumchota kuingia chama fulani lakini yeye hakuwa tayari kutokana na kazi yake ya biashara ambayo anahisi ndiyo muhimu zaidi.
“Mimi ni mfanyabiashara, kujikita na siasa kiukweli siwezi ila siyo kama sijajiandikisha, nina ‘kichinjio’ changu na Oktoba 25 nitampigia kura yule ninayeona anafaa kuliongoza taifa letu ambaye kwa sasa ni siri yangu,” alisema Madam Rita.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.