Umati wa vijana ukiwa hauamini kutokea kwa kifo cha Abdul Bonge.
Meneja
wa TMK Wanaume Family, Yamoto Band na Diamond, Said Fella akiwaeleza
kinachoendelea baadhi ya mastaa waliofika msibani hapo.
Msanii wa filamu za Kibongo, Baba Haji, akiwaelekeza wenzake ulipo msiba.
Mdogo
wa marehemu Abdul Bonge, Bab Tale akihojiwa na Mwandishi Mwandamizi na
Mpigapicha Mkuu wa Magazeti ya Global Publishers, Richard Bukos.
Fella akiwaeleza jambo vijana wake.
Waombolezaji wakiwa na nyuso za huzuni msibani hapo.
Mdogo wa marehemu, Habib Uledi (kushoto) akimueleza jambo msanii wa filamu za Kibongo, William Mtitu.
Wasanii wa filamu za Kibongo, Baba Haji na Riyama Ally wakisalimiana kwa kimtindo.
Mchekeshaji Kitale a.k.a ‘Mkude Simba’ akiingia msibani huku akifuatiwa na mchekeshaji mwenzake, Stan Bakora.
Wasanii wa filamu za Kibongo wakisalimiana.
Mdogo wa marehemu aitwaye Idd ambaye alikuwa ndiye wa kwanza kuitwa baada ya kaka yake kuanguka.
Kitale na Baba Haji wakifurahia jambo baada ya kukutana.
KIFO cha mdau wa muziki nchini ambaye ni mwanzilishi na meneja wa
kundi la Tip Top Connection, Abdul Shaban Taletale, kilichotokea
Magomeni-Kagera jijini Dar es Salaam, jana jioni kimeendelea kuzua utata
kufuatia mtuhumiwa wa mauaji mtu aliyetajwa kwa jina la Nassoro Idd
kuingia mitini.
Akizungumza na mandao huu, Meneja wa Kundi la Tip Top Connection na
mdogo wa marehemu, Hamisi Shaban ‘Bab Tale’, alisema siku ya tukio Abdul
Bonge akiwa maskani ya Tip Top Connection iliyopo Magomeni-Kagera
alifuatwa na kijana mmoja na kuambiwa rafiki yake aitwaye Nassoro Idd
alikuwa akipigana na mkewe hivyo aliagizwa na mama yake Nassoro akamwite
ili awasuluhishe.
Muda mfupi baada ya kwenda kwenye ugomvi huo zilirudi taarifa kuwa Abdul Bonge ameanguka na kupoteza fahamu.
Bab Tale alisema walimpeleka Hospitali ya Saint Monica iliyopo
Manzese-Darajani lakini waliambiwa tayari ndugu yao alikuwa amepoteza
maisha. Kufuatia tukio hilo Nassoro ametorokea kusikojulikana lakini
mkewe anashikiliwa na jeshi la polisi.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa muda wowote kwenda Kijiji
cha Mkuyuni kilichopo Matombo mkoani Morogoro baada ya polisi
kukamilisha uchunguzi wa tukio hilo na kuwakabidhi mwili huo.
(PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY / GPL)
Note: Only a member of this blog may post a comment.